1163 wathibitisha kushiriki Maonesho Nanenane 2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema kuwa washiriki wapatao 1163 wamethibitisha kushiriki katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane 2025 ambayo Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni, mkoani Dodoma. “Kutakuwa na teknolojia za huduma za kisekta ambapo waoneshaji 753 wanatoka katika Sekta za Umma na Binafsi, washirika kutoka katika taasisi za nje…
