Tanzania kusaini mkataba ukaguzi miamala ya kimataifa
Serikali inatarajia kusaini mkataba ambao utaiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupata taarifa mbalimbali kutoka nchi 146 duniani ambazo zitasaidia katika kuongeza ufanisi wa ukaguzi wa miamala ya kimataifa. Hayo yamebainishwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, aliyetaka kujua…
