Watanzania kujengewa uwezo kwenye teknolojia uchimbaji na uchenjuaji madini
Serikali ya Tanzania na Canada imepanga kuwajengea uwezo wataalamu na wachimbaji wa madini nchini Tanzania katika matumizi ya teknolojia ya kisasa ya uchimbaji na uchenjuaji madini. Hayo yameelezwa wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Ahmed Hussein na Waziri wa Madini wa Tanzania Anthony Mavundeyaliyofanyika Machi 04, 2025 Toronto, Canada…
