Umaskini, ukosefu wa maendeleo miongoni mwa changamoto Afrika
Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo umasikini, ukosefu wa maendeleo, ajira, amani na usalama na kutokuwa na sauti moja katika majukwaa ya kimataifa. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa Shaib amesema hayo wakati akifungua Semina ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka…
