Serikali yaanza mazungumzo ujenzi daraja Dar-Zanzibar
Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC), ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalounganisha Tanzania Bara na Zanzibar. Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema hayo bungeni Dodoma Aprili 28, 2023 kuwa mazungumzo hayo yalianza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi…
