Dkt. Biteko ataka mitungi gesi ya kupikia ifike ngazi ya vijiji
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Kampuni zinazohusika na Usambazaji wa Gesi za Mitungi Tanzania (LPG) -TZLPGA ambapo wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo kufikisha mitungi ya gesi ya kupikia hadi ngazi ya vijiji. Mazungumzo hayo yamefanyika Februari 20, 2025 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu…
