Zanzibar yahamasisha wawekezaji wazawa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji wanaowekeza nchini kwa kusimamia misingi na sheria za uwekezaji ili kuinua uchumi wa nchi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga amesema hayo wakati akifungua duka la vifaa vya kielektroniki. Amesema hatua hiyo itasaidia serikali kuongeza mapato…
