Sekta ya madini yafikia mchango wa 10.1% Pato la Taifa
Wizara ya Madini imetangaza kuwa Sekta ya Madini nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ya kihistoria kwa kufikia mchango wa asilimia 10.1 katika Pato la Taifa mwaka 2024, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya lengo lililowekwa kwenye Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026). Hayo…
