Sh milioni 200 zimetengwa majukwaa ya wanawake

kk

Shilingi milioni 200 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia majukwaa ya wananake kwa mwaka 2023/2024.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema hayo jijini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Subira Mgalu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katika swali lake la msingi, Mgalu alitaka kujua ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Mabaraza ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.

Kigahe amesema Serikali imekuwa ikiendesha Majukwaa (siyo Mabaraza) ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi tangu mwaka 2017.

Amesema lengo kuu la Majukwaa hayo ni kuwakutanisha wanawake ili waweze kujadili fursa za kiuchumi na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi nchini.

Amesema hadi kufikia mwaka 2021/2022, Mikoa yote 26 imezindua Majukwaa ya wanawake.

Amebaibisha kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga zaidi ya Sh milioni 72 na kwa mwaka 2023/ 2024 imetenga Sh milioni 200 kwa ajili ya uendeshaji wa majukwaa hayo.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks