WhatsApp Image 2023 08 31 at 13.52.28

Kampuni ya Urusi kununua matunda Tanzania

Kampuni ya Magnit ya nchini Urusi imeeleza nia ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania ikiwemo matunda. Hayo yameelezwa katika mkutano ulioratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kati ya kampuni hiyo na kampuni za Tanzania. Mwakilishi wa Kampuni hiyo ameeleza kuwa wanayo nia ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania ikiwemo ndizi, nanasi, embe,…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 08 22 at 12.20.02

Tanzania, Indonesia zasaini mikataba saba

Serikali ya Tanzania imeridhia uamuzi wa Serikali ya Indonesia kufufua shughuli za Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima (FARTC) kilichopo Mkindo mkoani Morogoro. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Joko Widodo aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi. Rais Samia amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 08 22 at 12.39.52

Tanzania kuacha kusafirisha korosho ghafi 2026/27

Serikali ya Tanzania imeazimia kuacha kusafirisha korosho ghafi ifikapo mwaka 2026/27. Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema hayo Agosti 21, 2023 wilayani Mkuranga alipotembelea kiwanda cha TANCOM kinachojihusisha na ukamuaji mafuta ya maganda ya korosho (CNSL) na kiwanda cha SABAYI INVESTMENTS cha kubangua korosho. Ameeleza kuwa mkakati wa Serikali ni kubangua korosho zote zinazozalishwa…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 08 18 at 11.45.58

Halmashauri 31 zapatiwa vifaa vya kupima afya ya udongo

Jumla ya Halmashauri 31 zimepatiwa vifaa vya kupima afya ya udongo kwa wakulima (Soil Scanner). Vifaa vilivyogaiwa ni soil scanner, vishikwambi, printer, lamination machine pamoja na seti ya kompyuta katika Halmashauri za mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Singida na Tabora. Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt….

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 08 18 at 11.45.40

Uzalishaji miche ya mkonge kwa chupa kufikia milioni 10

Serikali imepanga kuzalisha miche milioni kumi kwa njia ya teknolojia ya chupa (Tissue Culture) kupitia maabara ya kisasa inayojengwa katika Kituo cha Utafiti TARI Mlingano, Wilaya ya Muheza, Tanga. Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amebainisha hayo alipotembelea kituo cha TARI Mlingano na kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara hiyo. “Mahitaji ya miche ya mkonge…

Soma Zaidi
Enable Notifications OK No thanks