Makalla amuombea Rais Samia jina miradi DSM

WhatsApp Image 2021 07 06 at 16.11.58

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameomba jina la Rais Samia Suluhu Hassani liwekwe kwenye miradi ijayo ili kuwepo na kumbukumbu.

Miradi mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo madaraja makubwa na barabaraa imeandikwa majina ya viongozi.

Makalla ametoa ombi hilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa daraja la Tanzanite lenye urefu wa km 1.03.

Makalla amesema “niwie radhi na mimi ninaombi, nimeona nikusemee niombe jina lako liwekwe kwenye miradi mingine ijayo ya DSM. tumeona majina ya viongozi mbalimbali kama daraja la kijazi, daraja la mfugale na mengine mbalimbali.”

Aidha amempongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema miradi hiyo inasaidia wazawa.

Soma zaidi: Daraja la Tanzanite kuanza kutumika February Mosi


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks