Kijani Bond kutoa Riba ya 10.25%

WhatsApp Image 2023 08 31 at 17.47.10

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amezindua uuzaji wa hatifungani ya kijani “Kijani Bond” ya benki ya CRDB yenye riba ya 10.25%.

Taarifa ya CRDB inasema Kijani Bond inatoa fursa kwa watu wote kuwekeza kuanzia Sh. laki 5 kwa riba ya asilimia 10.25 kwa mwaka.

“Katika hatua hii ya mwanzo benki inatarajia kukusanya Sh. bilioni 55 zitakazoelekezwa kufadhili miradi inayotunza mazingira na kuzingatia mabadiliko yaa tabianchi,” imesema taarifa hiyo.

Kijani Bond ni hatifungani ya kwanza ya kijani Tanzania , na ya kwanza kwa ukubwa kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hatifungani hiy, inatoa fursa ya uwekezaji kwa muda wa miaka 5 ikiwa na thamani ya dola za Marekani milioni 300 sawa na Sh. bilioni 780.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks