Rais Mwinyi: Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa amani na utulivu 

WhatsApp Image 2025 04 04 at 14.57.12

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wananchi kuwa Uchaguzi Mkuu Ujao Utafanyika kwa Amani na Utulivu.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipotoa Salamu baada ya Kujumuika kwa Sala ya Ijumaa Masjid Raudha Uliopo Darajabovu, Mkoa wa Mjini Magharibi Aprili 4, 2025.

WhatsApp Image 2025 04 04 at 14.57.24

Amesema kuwa dhamira ya Serikali anayoiongoza ni kuona uchaguzi huo kuwa ni kielelezo cha kuwepo kwa Amani ya kudumu hapa nchini na kila mwananchi anapata fursa ya kutekeleza haki ya msingi ya Kikatiba ya kupiga kura.

Rais Dkt. Mwinyi amesema ni wajibu wa msingi wa kila mwananchi kuhakikisha amani iliopo inadumishwa  wakati huu na baada ya uchaguzi ili nchi ipige hatua zaidi za maendeleo katika nyanja tofauti.

Aidha amewanasihi waumini wa dini ya Kiislamu  kuendeleza utaratibu wa kuwasaidia watu wanaohitaji misaada kama ilivyofanyika vema wakati wa Mwezi wa  Ramadhani.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi ameeeleza kuwa mwenendo mzuri uliotekelezwa wakati wa Ramadhani unapaswa kuendelezwa kwa kiwango kile kile kwani bado makundi ya wanaohitaji kusaidiwa yapo ndani ya Jamii.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks