Utalii waingiza Bilioni 522.7 mwaka 2022/23
Sekta ya utalii Tanzania imevunja rekodi kwa kuingiza Shilingi Bilioni 522.7 katika mwaka 2022/2023. Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa amesema fedha hizo zimetokana na watalii 1,638,850 kutoka nje waliotembelea Tanzania kwa kipindi hicho. “Sekta ya utalii imevunja rekodi kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa ongezeko ambalo halijawahi kutokea, tumshukuru sana Rais Dk. Samia…
