Home Elimu Walimu Afrika wanawezaje kuunda mustakabali wa bara hili?

Walimu Afrika wanawezaje kuunda mustakabali wa bara hili?

0 comments 317 views

Katika miaka 25 ijayo, idadi ya watu barani Afrika inatarajiwa kuongezeka mara mbili na kufikia bilioni 2.5 – sawa na robo moja ya idadi ya watu wote duniani. Walimu barani Afrika wanategemewa zaidi juu ya mustakabali wa bara hili.

Makadirio haya yanatarajiwa kuwa na faida nyingi ikiwemo kukua kwa masoko, uvumbuzi na kuongezeka kwa uzalishaji.

Jibu la swali hili litategemea uwezo wa bara hili kutumia rasilimali watu kukabiliana na vikwazo vya kimuundo. Watunga Sera katika ukanda wa Afrika wanajikita katika masuala ya ukosefu wa ajira, ukuaji wa miji pasipo mapinduzi ya viwanda na pengo la kidijitali linalozidi kuongezeka.

Changamoto za maendeleo duni, kutokuwepo kwa uafanisi wa mageuzi ya elimu, ukosefu wa ajira na mapinduzi ya viwanda zilizorithiwa kutoka kwa mifumo ya ukoloni ni changamoto zinazozikabili nchi nyingi barani Afrika.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inaonyesha hali hii. Vikwazo vya kiuchumi vya Kanda, vimekuza idadi kubwa ya vijana, ikionyesha kuongezeka kwa nguvu kazi katika miongo ijayo. Katika muktadha huu, shule za Afrika Mashariki zinaweza kuwa taasisi muhimu zaidi. Lakini je, mifumo yao ya elimu inakua kwa kasi?  Na walimu wao wako tayari kwa kiasi gani katika uhamasishaji chanya?

Nchini Kenya, Uganda, na Tanzania, ufahamu wa mambo yajayo unachochea mageuzi. Kuhamia katika “Mtaala wa Kuzingatia Uwezo” (Competency-Based Curriculum CBC) – ambao lengo lake ni kuhama kutoka kwenye kupata maarifa hadi kuyatumia – elimu imekuwa inalenga zaidi ujuzi, na walimu wanatambuliwa kuwa kiunganishi muhimu katika kufanikisha mageuzi haya.

Mfano wa Kenya unaonyesha jinsi walimu wanavyoweza kutumika kama mawakala wa mageuzi.

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa CBC mwaka 2017, zaidi ya walimu 300,000 wamepata mafunzo ya kuhama kutoka kwenye kujifunza kwa kukariri hadi kwenye mbinu za inayomlenga mwananfunzi.  Tume ya Huduma kwa Walimu pia imezindua mpango wa Maendeleo ya Kitaaluma kwaWalimu, unaolenga kuboresha ujuzi wa walimu.

Chini ya mpango huu, warsha za mafunzo ya walimu zinalenga kuboresha ufundishaji, kukuza ujumuishwaji, na kuzingatia mahitaji ya mwanafunzi. Kama alivyosema Anne Gachoya, Naibu Mkurugenzi wa Elimu katika Wizara ya Elimu ya Kenya: “Walimu wenye mafunzo bora humaanisha matokeo bora.”

Tanzania inatoa mfano mwingine wa kufundisha. Baada ya kuanzishwa kwa elimu ya msingi bila malipo mwaka 2016, idadi ya wanafunzi iliongezeka kwa kasi na kuleta utofauti kati ya madarasa, walimu na wanafunzi. Katika kukabiliana na hilo na kwa lengo la kuboresha mafunzo ya walimu, serikali ilizindua “Mafunzo Endelevu kwa Walimu Kazini) unaojulikana kama MEWAKA.

Mpango huu, unaosaidiwa na Benki ya Dunia (WB) na washirika wengine, unawaandaa walimu kwa mafunzo ya msingi, fursa za uongozi na mbinu za kujifunza kidigitali. Kwa kuipa kipaumbele mbinu ya kujifunza kwa vitendo, MEWAKA inalenga kubadilisha ushiriki wa walimu katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za ufundishaji.

Matokeo ya awali ya mpango huu, yalionesha kuimarika kwa ushiriki darasani baina ya mwalimu na mwanafunzi.

Uganda pia inafanya maendeleo mazuri. Kukabiliana na matokeo duni ya uwezo wa kusoma na kuandika, nchi hiyo ilijitolea kutoa mafunzo kwa walimu wa darasa la awali kwa kutumia mbinu za sauti kw akutumia lugha za kienyeji katika eneo husika. Katika baadhi ya wilaya, uwezo wa wanafunzi kusoma umeongezeka mara mbili zaidi.

Kama ilivyo kwa majirani zake, Uganda pia imelazimika kukabiliana na matatizo ya kimfumo kama vile madarasa makubwa, miundombinu duni, na upungufu wa walimu shuleni. Utafiti wa Benki ya Dunia unaonyesha kuwa upungufu wa walimu nchini Uganda ni kati ya wastani wa asilimia 27-30.

Hata hivyo, ingawaje kila nchi inakabiliana na changamoto na fursa tofauti katika elimu, upo mtazamo unaofanana Afrika Mashariki: mafanikio ya mageuzi ya mitaala yanategemea si tu sera pekee, bali pia watu – wana taaluma – wanaotekeleza. Uwezo wa walimu kufanya mageuzi katika ufundishaji ndio utabainisha kama wimbi la idadi ya watu linaweza kuleta mafanikio kiuchumi.

Hapa ndipo mipango kama Schools2030 inapoingia. Kama mpango wa miaka 10 unaofanyika katika nchi 10 (ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, na Uganda), na kuongozwa na Aga Khan Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine, Schools2030 inajitolea kuwawezesha walimu na jamii kutika mazingira yao.

“Kiini cha Schools2030 ni kuzingatia uwezo wa walimu, kuwatambua walimu kama viongozi, wabunifu, na watekelezaji wa mageuzi ya elimu,” anasema Halima Shabaan, Mratibu wa Kitaifa wa Schools2030 nchini Kenya.

Kwa kushirikiana na serikali, Schools2030 imewapa walimu jukwaa la kusikika na kutambuliwa kwa kushirikishana habari za mabadiliko na maboresho.

Hii imesaidia kuonesha kuwa walimu kote Afrika Mashariki wanakabiliwa na changamoto ya kufundisha na kufanya maamuzi.

Kwa mfano, mwalimu mmoja nchini Kenya ameunda “Speak-up Spot” – sanduku ambapo wanafunzi wanaweza kuweka maoni yao kwa maandishi bila kujulikana ni nani ameandika. Maoni hayo hujadiliwa kwa kushirikisha wazazi na kuja na mrejesho katika nyanja ya elimu na kihisia na kuimarisha ushiriki wa wazazi katika suala la elimu.

Uvumbuzi mwingine unaenea mipakani kote. Kifaa cha kusoma na kuandika kilichobuniwa Tanzania, kinachojulikana kama “T-Learning”, kimekubaliwa kutumika katika maeneo mengine ya ukanda. Kwa mfano, walimu wa Kenya wameubadili mfumo huo na kuutumia kufundisha masomo mengine kama Sayansi.

Wakati Afrika Mashariki inafanya kila linalowezekana pale walimu wanapowekwa katika nafasi muhimu kwenye mageuzi ya elimu, bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Utendaji wa leo katika mifumo ya elimu, ni kiini cha matokeo ya kiuchumi na kijamii baadaye.

Nguvu kazi kubwa ya watu wenye elimu ni kivutio cha uwekezaji na kuongeza ukuaji wa uchumi. Kinyume chake, ikiwa elimu itashindwa, hatari za umaskini, ukosefu wa ajira kwa vijana, na machafuko ya kisiasa vinaweza kutokea.

Lengo ni kuhakikisha kuwa ushawishi ujao wa Afrika sio tu kwa idadi yake ya watu, bali pia kwa elimu ubora na ubunifu wa viongozi wake.

Wakati viongozi wa elimu, wataalamu, na waanda sera wanakutana jijini Nairobi kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Schools2030 kuanzia Juni 3 hadi 5, majadiliano kuhusu ongezeko la idadi ya watu barani Afrika – na jinsi mifumo yetu ya elimu inaweza kusaidia kufanikiwa, huu ni muda muafaka.

Makala hii ilichapishwa Daily Monitor.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!