Home Elimu Takribani bilioni 1.6 zachangwa kongamano la eLearning Afrika

Takribani bilioni 1.6 zachangwa kongamano la eLearning Afrika

0 comments 273 views

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ameongoza Harambee maaalum ya wadau mbalimbali kuchangia Kongamano la eLearning Africa ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6 zimepatikana.

Akizungumza Aprili 16, 2025 jijini Dar es Salaam katika Harambee hiyo kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania kwa mara nyingine inaingia katika historia ya kimataifa kwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la Kimataifa ambalo lina manufaa makubwa katika taifa na kipekee katika kuimarisha sekta ya Elimu.

Amesema hakuna namna Tanzania itakwepa matumizi ya TEHAMA na teknolojia mbalimbali katika mifumo ya utoaji elimu bali ni kuhakikisha tunaenda sambamba na maendeleo hayo.

Ameongeza kuwa Tanzania kuwa mwenyeji wa kongamano hilo kunatokana na ukweli kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amieweka nchi yetu katika ramani kupitia uimarishaji wa Diplomasia ya kimataifa, hatua hiyo imechochea ukuaji wa sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii.

Amewashukuru wadau wote waliojitokeza kuchangia na kuendelea kuhimiza wengine kujitokeza kuchangia na kushiriki katika hatua mbalimbali ikiwemo kuwezesha wanafunzi na wabunifu wachanga kushiriki.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukuza bunifu na teknolojia ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika elimu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Hivyo kupitia kongamano hilo wadau zaidi ya 1,500 wakiwemo Mawaziri wa Elimu kutoka Nchi zaidi ya 50 watashiriki kujadiliana mwelekeo huo.

“Mhe. Mgeni rasmi nasi hatuko nyuma tayari tuna Mkakati na miongozo ya matumizi ya teknolojia katika elimu ikiwemo matumizi ya Akili Unde, hivyo vijana, wabunifu Taasisi, Vyuo na mashirika jiandikisheni kushiriki katika kongamano, maonesho na mijadala itakayoendeshwa”

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema tukio hilo linaonesha uwezo wa nchi katika kuandaa mikutano ya kimataifa, pamoja na kuakisi dhamira ya serikali ya kuwekeza katika elimu na teknolojia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!