Chuo Kikuu Mzumbe chashauriwa kufadhili wahitimu

sawawa

Wito umetolewa kwa uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe (MU) kuanzisha mfuko wa ufadhili wa wahitimu wa Chuo hicho “ Alumni Scholarship Scheme”.

Uazishwaji wa mfuko huo utawasaidia Watanzania ambao wana sifa ya kusoma katika ngazi ya Chuo Kikuu lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanakosa hiyo fursa muhimu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, ametoa wito huo katika mkutano mkuu wa 22 wa Baraza la Masajili la Chuo Kikuu cha Mzumbe uliofanyika  katika ukumbi wa Maekani uliopo Kampasi kuu ya Chuo hicho  mkoani Morogoro.

Amesema mfuko huo utasaidia wanafunzi wanaongia  chuoni  na kushindwa kuendelea na masomo yao  kutokana na ukosefu wa fedha.

Hemed ameeleza kuwa yenye ni mmoja kati ya waliosoma chuoni hapo  na kusema uanzishwaji wa mfuko utasadifu kauli mbiu ya Chuo kikuu hicho inayosema  “ Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu”.

Amesema Chuo kikuu hicho ni kati ya  Vyuo vikuu  nchini vinavyofanya vizuri kwa kutoa viongozi wa ngazi ya juu ikiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na wengine waliopo serikalini na sekta binafsi.

Hemed pia ameushauri  uongozi wa Chuo kuangalia namna ya kuanzisha ushirikiano na Vyuo vya Zanzibar ili kutanua wigo wa kuchagua Program za kujiufunza na kusogeza fursa ya elimu kwa Wazanzibari.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks