Wanawake 200 wapata mafunzo ya biashara

nbc

Takribani wanawake 200 wamepata mafunzo ya biashara yaliyolenga kuwajengea uwezo.

Mafunzo hayo yametolewa  na benki ya NBC kwa wafanyabiashara katika kipindi cha maonesho ya Viwanda kwa Wanawake wajasiriamali kwa mwaka 2022.

Neema Rose Singo amabae ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC amesema “tumetoa mafunzo kwa wanawake wafanyabiashara takribani 200, na tunaamini mafunzo haya yataongeza tija katika uendeshaji wa biashara zao katika kipindi kifupi kijacho.
Ameeleza kuwa benki ya NBC ina huduma mbalimbali zinazowalenga wanawake wajasiriamali ikiwemo akaunti ya Johari ambayo ni maalumu kwa wakina mama ambao wanania ya kuweka akiba ya uwekezaji wa baadae wakati huo mmiliki akipatiwa riba hadi kufikia asilimia 7 pamoja na mikopo bila ya dhamama”.

Katika hafla hiyo, zilitolewa tuzo kwa washindi wa Tuzo za Viwanda kwa wanawake wajasiriamali.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks