Japan yaipa Tanzania bilioni 68.5

WhatsApp Image 2024 10 18 at 14.50.37

Tanzania imepokea msaada wa yen bilioni 4.07 sawa na Shilingi bilioni 68.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa ndani katika Jiji la Dodoma.

Msaada huo umetolewa October 18, 2024 na Japan, kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA).

Mkataba wa Msaada huo umetiwa Saini katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa upande wa Tanzania, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa na Mwakilishi wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA), Hitoshi Ara.

Mradi huu utahusisha Utanuzi wa barabara kutoka njia mbili hadi nne kuanzia mzunguko wa barabara ya Bahi (BAHI Round About) hadi Image na ujenzi wa barabara mpya njia nne kuanzia mzunguko wa barabara ya Image (Image Round About) hadi mzunguko wa barabara ya Makulu (Makulu Round About).

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, Maafisa waandamizi kutoka Wakala wa Barabara-TANROADS, na maafisa wengine wa Serikali kutoka Tanzania na Japan.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks