Deni la Serikali lafika Sh 69.44 trilioni
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa Sh69.44 trilioni ikilinganishwa na Sh60.72 trilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2021, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 14.4. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani Sh22.37 trilioni na la nje ni Sh47.07 trilioni. Dk Nchemba amebainisha…
