Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, kodi: Mwigulu
Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi. Dkt. Nchemba ameyasema hayo Agosti 20, 2024 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake…
