Shilingi bilioni 743.57 zapatikana mauzo ya korosho kwa wiki nne
Wakati minada ya korosho katika msimu wa 2024/2025 ikiendelea, Mkurugezi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred amesema kuwa jumla ya Tsh bilioni 743.57/= zimepatikana katika wiki nne za minada ya korosho. Alfred ameeleza hayo Novemba 4, 2024 wakati akizungumza na wandishi wa habari. Huku wakulima zaidi ya asilimia 90 wakiwa wamelipwa fedha zao,…
