Bashe azitaka nchi za SADC kushirikiana kuzalisha chakula
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa rai kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kushirikiana kuzalisha chakula kwa mpango ambao kila nchi itanufaika. Bashe ameyasema hayo Julai 3, 2023 wakati akiwasilisha mada kuhusu kilimo cha kisasa kama njia ya kukabiliana na upungufu wa chakula katika mkutano wa 53 wa Mabunge ya SADC…
