Ukuaji kilimo kufika 10% ifikapo 2030
Serikali inaendelea na utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini ikiwemo Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (5), (FYDP III) na Ajenda 10/30 ambayo inalenga kuchochea ukuaji wa kilimo kufikia asimilia 10 ifikapo mwaka 2030. Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amesema hayo Februari 16, 2024 bungeni jijini Dodoma. Amesema…
