Mvinyo wa mlonge, asali watengenezwa Kibaha
Umewahi kuona mvinyo wa majani ya mlonge na asali? “Huu ni mvinyo (wine) uliotengenezwa kwa majani ya mlonge na asali. Mvinyo huu huvundikwa kiasili kwa muda wa mwezi mmoja hadi miezi mitatu,” anaeleza Bahati Malangalila, Mkurugenzi wa One Love Naturals. Malangalila ambae awewahi kufanya kazi kwa miaka 15 katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),…
