Marekani, Kenya zaongoza utalii Tanzania
Marekani na Kenya zimetajwa kuwa ndio nchi zinazoongoza kwa watalii wanaotembelea Tanzania. Utalii wa Tanzania umeanza kuongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari mpaka Julai mwaka huu Tanzania imepata watalii 742,133 sawa na ongezeko la asilimia 62.7 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana ambapo kulikuwa na watalii 456,266. Kati ya watalii 742,133 walioingia nchini,…
