Home KILIMOKILIMO BIASHARA Tanzania ya pili uzalishaji mbaazi duniani

Tanzania ya pili uzalishaji mbaazi duniani

0 comments 196 views

Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa zao la mbaazi duniani baada ya nchi ya India.

Akiwasilisha mwenendo wa zao la mbaazi nchini kwa Mwaka 2024/2025, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( COPRA) Irene Mlola amesema uzalishaji wa mbaazi nchini umeongezeka hadi kufikia Tani 307,000 kwa msimu uliopita na kuiweka Tanzania kwenye nafasi ya pili ya uzalishaji wa mbaazi duniani.

Amesema urasimishaji wa mifumo ya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko umeleta matokeo chanya kwenye maendeleo ya uzalishaji na mnyororo wa biashara ya zao la mbaazi nchini.

Tanzania ya pili uzalishaji mbaazi duniani pesatu.comMkurugenzi Mlola amesema katika kuunga mkono juhudi za wakulima nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametumia diplomasia ya kiuchumi kama njia ya kufungua masoko ya mazao ya wakulima.

Amefafanua kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara nchini India, ziara ambayo imeleta fursa ya mbaazi zinazolimwa na wakulima wa Tanzania kuingizwa nchini India bila ushuru wa forodha (Import free regime) hatua ambayo inaleta tija kwenye kilimo cha mbaazi na kuhamasisha wakulima kuzalisha zaidi na kupelekea uzalishaji wa mbaazi Tanzania kupanda hadi kufikia tani 400,000 msimu huu ikilinganishwa na uzalishaji wa tani elfu 90 katika miaka minne iloyopita.

Ameongeza kuwa mifumo ya stakabadhi za ghala na minada ya kidigitali imewasaidia wakulima kusogezwa karibu na soko na kuongeza wigo wa wanunuzi kushiriki kwa uwazi na hatimaye kupata bei zenye ulinganishi wa moja kwa moja na bei zilizopo kwenye soko la kimataifa.

“Bei ya mkulima imekua na ulinganishi na soko la kimataita kupitia mifumo ya kidijitali. Tofauti ya bei ya Mkulima na bei ya soko la Kimataifa ilikua chini kufikia asilimia 25. Kwa mfano Mwaka 2022/2023 Wakulima waliuza kati ya Sh. 200 mpaka Tsh. 500, wakati Soko la India lilinunua kwa zaidi ya Tsh. 2,200 lakini Sasa mkulima wa Tanzania anapata zaidi ya asilimia 66 ya bei ya soko la dunia”. Amesema Mkurugenzi Mkuu Mlola.

Mkurugenzi Mkuu Mlola ameshiriki kwenye Mkutano wa Wadau wa zao la Korosho uliofanyika jijini Dodoma na kupata fursa ya kuwasilisha mwenendo wa zao la mbaazi nchini kwa mwaka 2024/2025.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!