Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Kama unafanya biashara ya miwani hii inakuhusu

Kama unafanya biashara ya miwani hii inakuhusu

0 comments 205 views

Uuzaji wa miwani kiholela umeshamiri katika maeneo mengi nchini husasani mijini. Miwani hizo nyingi zikiwa ni zile zinazotajwa kuwa ni miwani za urembo.

Mbali na kumsababishia madhara mtumiaji anayetumia miwani pasipo kuipima na kupima macho yake, pia mtu yeyote anayejihusisha na biashara ya miwani anatakiwa azingatie sheria ya Optometria sura namba 23 ikiwemo kusajiliwa katika Baraza la Optometria.

Hayo yamebainishwa na timu ya Usimamizi Shirikishi ikiongozwa na Msajili wa Baraza la Optometria nchini. Sebastiano Millanzi.

Baraza la Optometria limeendesha elimu ya matumizi sahihi ya miwani ili kuwaepusha watu kujinunulia miwani kiholela.

Elimu hiyo imetolewa Agosti 18, 2025 katika Soko la Kabwe lililopo jijini Mbeya ambapo imebainika kuwepo kwa baadhi ya wafanyabishara ambao hawana taaluma ya Optometria lakini wanajihusisha na uuzaji wa miwani bila kuwapima na kuiuza pamoja na bidhaa nyingine mbalimbali za urembo kinyume na miongozo iliyopo.

Kama unafanya biashara ya miwani hii inakuhusu pesatu.com

Msajili wa Baraza la Optometria Sebastiano Millanzi akitoa elimu kwa wafanyabiashara jijini Mbeya

Akitoa elimu wakati wa zoezi hilo Msajili wa Baraza la Optometria Sebastiano Millanzi amesema miwani ni miongoni mwa tiba, hivyo kuziuza kiholela zinaweza kuleta athari kwa mtumiaji, ni vema anayetaka kujihusisha na biashara ya miwani azingatie sheria ya Optometria sura namba 23 ikiwemo kusajiliwa katika Baraza hilo.

“Kutokujua sheria sio sababu ya kuvunja sheria na ni bahati kuwa ninyi mlikuwa bado hamjapata elimu hii, hivyo kwa sasa tunawapa elimu pamoja na kuwataka kusitisha hadi pale mtakapokamilisha taratibu stahiki za usajili kuanzia ngazi ya Mganga Mkuu wa Jiji,” amesisitiza Millanzi.

Kwa upande wao wafanyabiashara hao wamekiri kufanya biashara hiyo bila kujua kuwa wanakiuka taratibu, hivyo wakaahidi kuzingatia maagizo yaliyotolewa kwao ya kuanza taratibu za usajili.

Millanzi ametumia wasaa huo kuziagiza mamlaka za usimamizi ngazi ya Halmashauri na Mkoa kuwa na muendelezo wa usimamizi shirikishi wa mara kwa mara na kutoa elimu endelevu kwa wananchi.

Timu ya usimamizi kutoka Wizara ya Afya chini ya Baraza la Optometria inashirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, ngazi ya mkoa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika kazi hiyo.

Kutumia miwani bila kufanyiwa uchunguzi wa macho na daktari (optometrist au ophthalmologist) kunaweza kuleta madhara kadhaa, kama ifuatavyo:

Kutumia nguvu isiyo sahihi inayosababisha macho kuchoka

Miwani yenye presha isiyo sahihi inaweza usababisha maumivu ya kichwa, macho kuchoka kutokana na kutumia nguvu kubwa kutanua misuli ya macho ili kuweza kuona.

Dalili zingine ni macho kukauka, kizunguzungu, na kupata ugumu wa kutizama kitu kwa umakini.

Kuathiri zaidi uono wako

Miwani yenye presha kali mno au dhaifu mno inaweza kuharibu zaidi uono wako, hasa kwa watoto na vijana.

Watu wenye astigmatism au macho duni (amblyopia) uono wao unaweza kudhoofika zaidi kama hawajachunguzwa kwa ufasaha.

Kuficha magonjwa mengine

Baadhi ya matatizo ya kuona yanaweza kuwa dalili za magonjwa mengine makubwa kama glaucoma, mtoto wa jicho au kisukari.

Kujipatia miwani bila kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu kunaweza kusababisha kuchelewa kupata matibabu ya magonjwa mengine ambayo dalili zake huonekana pia katika magonjwa ya macho.

Kama unafanya biashara ya miwani hii inakuhusu pesatu.com

Miwani isivyo na mwelekeo sahihi inaweza kuumiza

Miwani isiyo na vipimo sahihi (kama umbali wa pupils) inaweza kusababisha kuona mara mbili au kutoana sawa sawa.

Miwani ya bei rahisi au ya hali ya chini inaweza kusababisha macho kuumia kutokana na mwanga mkali.

Inaweza kuongeza au kusababisha ajali

Unaweza ukatumia miwani na ukaona vizuri, ingawaje miwani hiyo inakuwa sio sahihi hivyo unaweza kupelekea kokosa makadiria sahihi ya umbali au kuchelewa kujibu na hivyo kuongeza hali ya hatari ikiwemo kuanguka au kupata ajali nyingine hususani kwa wale wanaoendesha vyombo vya moto.

Usitumie miwani ya macho bila uchunguzi

Miwani ya kusomea (yenye kuongeza ukuaji wa herufi) inaweza kutumika kwa urahisi ikiwa ni ya nguvu ndogo (+1.00 hadi +2.50) na kwa muda mfupi tu.

Miwani ya kuzuia mwanga wa bluu (isiyo na nguvu/lensi) inaweza kusaidia kupunguza macho kuchoka kwenye vifaa vya kidijitali na mwanga mkali lakini haitasaidia kurekebisha tatizo la uono.

Nini cha kufanya ili uweza kujiepusha na matatizo ya macho:

Pima macho yako kila baada ya mwaka mmoja au miwili. Unaweza kupima mara kwa mara kama una ugonjwa wa kisukari au kama mna historia katika familia ya kuwa na matatizo ya macho.

Epuka kununua miwani ya kutibu maho kabla ya kupata uchunguzi wa daktarin wa macho.

Mwone daktari mara tuu unapohisi mabadiliko ya uono wako kama vile mwanga au vidonda machoni.

Kutumia miwani isiyo sahihi kunaweza kuonekana kama hakuna shida,lakini kadri muda unavyozidi kwenda inaweza kukuleta matatizo ya macho na maumivu. Kwa hivyo, ni bora kuonana na mtaalamu wa macho kabla ya kununua miwani hususani zenye lensi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!