Home Elimu ZAIDI YA WATU MILIONI MOJA WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA

ZAIDI YA WATU MILIONI MOJA WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA

0 comments 275 views

Idadi ya walioambukizwa virusi vya Corona duniani imefikia watu milioni moja ishara ya kupanda kwa kasi kiwango cha maambukizi ndani ya kipindi cha wiki chache zilizopita.Katika muda wa wiki moja iliyopita visa vingi vya virusi vya Corona vimerikodiwa duniani ikilinganishwa na muda wa karibu miezi mitatu tangu virusi hivyo vilipogunduliwa kwa mara ya kwanza.Takwimu zilizikusanywa pia zinaonesha idadi ya vifo imefikia watu 51,178 ambayo ni maradufu ya vifo vilivyorikodiwa hadi tarehe 27 mwezi Machi.Bara la Ulaya ndilo kitovu cha virusi vya Corona ambako mataifa ya Italia na Uhispania yameathirika zaidi kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa COVID-19.Hata hivyo kumekuwa na ishara ya kupungua kiwango cha maambukizi nchini Italia kutoka asilimia 18 hadi asilimia 5 ya visa vinarikodiwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Pesatu ni jukwaa la habari, elimu ya kifedha, na ujasiriamali Tanzania. Tunakuletea taarifa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, kilimo, mitindo, na burudani, pamoja na mwongozo wa kufanikisha mafanikio yako. Kwa makala zetu, mwongozo wa vitendo, na taarifa za hivi punde, tunasaidia wajasiriamali, vijana, na jamii kupata maarifa yanayoweza kubadilisha maisha yao na kuongeza fursa za kifedha.

Jarida la Habari

PESATU – Haki Zote Zimehifadhiwa. Imetengenezwa na Mediapix Limited