Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Kenya na Tanzania sio wapinzani : Rais Samia

Kenya na Tanzania sio wapinzani : Rais Samia

0 comments 354 views

Rais wa Tanzania, Samia suluhu Hassan amesema uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya hauwezi kuvunjika akibainisha kuwa  wapo watu wenye nia ovu wanaotamani kuona umevunjika.

Rais Samia amesema hayo Mei 5, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Kenya mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya.

“Ni bahati mbaya kuwa watu hawa wapo katika pande zote mbili, Kenya na Tanzania hutokea pia wachache wao wakawa ni watumishi wa Serikali zetu na hata wanasiasa. Binafsi huwa nashangazwa sana na wale wanaodhani Kenya na Tanzania ni wapinzani, mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumwangusha mwenzake,  hawa ni watu wenye mioyo ya choyo, maono mafupi na akili mbovu.”

Ameahidi katika uongozi wake atahakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa ndugu, jirani, mshirika wa mkakati na mbia kwa kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili umefungwa katika mafundo matatu.

Rais Samia amesema “panapotokea ukame Tanzania njaa inabisha hodi Kenya, uzalishaji wa viwanda ukisimama Kenya bidhaa zinakosekana Tanzania hivyo hatuna budi kupatana na kuishi kwa neema na furaha.”

Pesatu ni jukwaa la habari, elimu ya kifedha, na ujasiriamali Tanzania. Tunakuletea taarifa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, kilimo, mitindo, na burudani, pamoja na mwongozo wa kufanikisha mafanikio yako. Kwa makala zetu, mwongozo wa vitendo, na taarifa za hivi punde, tunasaidia wajasiriamali, vijana, na jamii kupata maarifa yanayoweza kubadilisha maisha yao na kuongeza fursa za kifedha.

Jarida la Habari

PESATU – Haki Zote Zimehifadhiwa. Imetengenezwa na Mediapix Limited