Home FEDHA TAMISEMI yakusanya trilioni 1.11/- 2024/2025

TAMISEMI yakusanya trilioni 1.11/- 2024/2025

0 comments 333 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema hadi Machi, 2025 Sh.Trilioni 1.11 zimekusanywa sawa na asilimia 93.15 ya lengo la kukusanya Sh.Trilioni 1.60 kwa Mwaka 2024/25.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2025/26, Waziri Mchengerwa amesema kati ya fedha hizo Sh. Tilioni 61.21 ni kodi ya majengo, Sh. Trilioni 1.04 ni mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa.

Pia, amesema Sh. Bilioni 16.23 ni mapato ya ndani ya taasisi na Sh. Milioni 201.60 ni maduhuli ya mikoa.

Amefafanua kuwa makusanyo hayo yalitokana na ada za wanachuo, tozo, ukusanyaji wa madeni, mauzo ya bidhaa mbalimbali na ushuru unaotozwa na mamlaka za serikali za mitaa kulingana na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290.

Mchengerwa amesema kwa kipindi hicho TAMISEMI ilipanga kutumia Sh. Bilioni 541.27 za mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hadi Machi, 2025 Sh.Bilioni 312.30 sawa na asilimia 57.70 zimetolewa.

Ameeleza kuwa baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa kipindi hicho ni ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, ujenzi wa barabara, machinjio, minada nyumba za walimu na watumishi wa afya, hospitali, vituo vya afya, zahanati, vituo vya polisi na ununuzi wa magreda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!