Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Rais Samia kuhutubia bunge kwa mara ya kwanza

Rais Samia kuhutubia bunge kwa mara ya kwanza

0 comments 349 views

 Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhamisi Aprili 22, 2021.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amelitangazia Bunge kuwa Rais Samia atalihutubia Bunge kuanzia saa 10 jioni.

Spika Ndugai amewaagiza wabunge wote walioko nje ya Jiji la Dodoma kurudi na wale wanaotaka kuondoka wazingatie kuwapo kwa shughuli hiyo kwanza.

Rais Samia atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

Pesatu ni jukwaa la habari, elimu ya kifedha, na ujasiriamali Tanzania. Tunakuletea taarifa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, kilimo, mitindo, na burudani, pamoja na mwongozo wa kufanikisha mafanikio yako. Kwa makala zetu, mwongozo wa vitendo, na taarifa za hivi punde, tunasaidia wajasiriamali, vijana, na jamii kupata maarifa yanayoweza kubadilisha maisha yao na kuongeza fursa za kifedha.

Jarida la Habari

PESATU – Haki Zote Zimehifadhiwa. Imetengenezwa na Mediapix Limited